“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

YANGA YAWASILI MBEYA KUWAVAA PRISONS KESHOKUTWA SOKOINE

KIKOSI cha Yanga kimewasili Jijini Mbeya kwa ndege leo jioni tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons keshokutwa Uwanja wa Sokoine.
Huo utakuwa mmoja kati ya michezo nane ya keshokutwa itakayoanza muda mmoja, Saa 10:00 jioni na yote kurushwa na chaneli mbalimbali za Azam TV – ikiwemo Simba SC watakaokuwa wageni wa Ken Gold Uwanja wa Ali Hassan mjini Tabora.
Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 73, moja zaidi ya Simba SC baada ya wote kucheza mechi 27.


Ligi Kuu inaingia katika Raundi ya 29 kabla ya kukamilishwa msimu katika Raundi ya 30 Juni 22 — lakini Simba na Yanga zina kiporo kwa mechi baina yao Juni 25 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambayo ndio inafarajiwa kuamua Bingwa wa msimu huu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button