“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

YANGA SC YAPANGWA ‘KUNDI LA KIFO’ LIGI YA MABINGWA AFRIKA, SIMBA WASHINDWE WENYEWE

MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wamepangwa Kundi B katika Hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wapinzani wote watatu kutoka nchi Kaskazini mwa Afrika.
Wapinzani hao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Al Ahly ya Misri, AS FAR Rabat ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria.
Timu nyingine ya Tanzania, Simba SC imepangwa Kundi D pamoja na Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia, Petro de Luanda ya Angola na Stade Malien ya Mali.
Kundi A liwakautanisha mabingwa watetezi, Pyramids FC ya Misri, mabingwa wa Kimbe la Shirikisho Afrika, RS Berkane ya Morocco, Rivers United ya Nigeria na Power Dynamos ya Zambia.
Kundi C linaundwa na mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan, MC Alger ya Algeria na St Éloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

RATIBA LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
Mechi za Kwanza: 21-23 November
Mechi za Pili: 28-30 November
Mechi za Tatu: 23-25 January
Mechi za Nne: 30 Janunary-01 February
Mechi za Tano: 06-08 February
Mechi za Sita: 13-15 February

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button