“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

YANGA PRINCESS WASHINDI WA TATU NGAO YA JAMII

TIMU ya Yanga Princess imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mashujaa Queens katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu michuano ya Ngao ya Jamii Wanawake mchana wa leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga Princess yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Jeannine Mukandayisenga dakika ya 16 na viungo, Mnigeria Precious Christopher dakika ya 48 na Muhabeshi, Aregash Kalsa dakika ya 65.
Wakati Mashujaa Queens ikifungwa 2-0 na Simba Queens katika mechi za Nusu Fainali, Yanga Princess ilitolewa na JKT Queens kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 1-1 hapo hapo KMC Complex.
Fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2025 itafuatia Saa 10:00 jioni hapo hapo KMC Complex baina ya ma-Queens wa Simba na JKT.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button