YANGA MPYA MOTO ULE ULE, YAITANDIKA RAYON 3-1 AMAHORO

KLABU ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Rayon Sports katika mchezo wa kirafiki kuhitimisha tamasha la Rayon Sports Day usiku huu Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali, Rwanda.
Haukuwa ushindi rahisi, kwani ilibidi Yanga watoke nyuma baada ya bao la kujifunga la beki Aziz Aziz Andambwile Mwambalswa dakika ya kwanza tu alipomrudishia pasi fyongo kipa Djigui Diarra raia wa Mali.
Hata hivyo, Yanga ilizinduka kwa mabao ya mshambuliaji mpya, Mkongo DR, Andy Bobwa Boyeli aliyesajiliwa kutoka Sekhukhune United FC ya Afrika Kusini dakika ya 28, kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua dakika ya 45 na beki Bakari Nondo Mwamnyeto dakika ya 90’+4.




Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga chini ya chini ya Benchi jipya la Ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Mfaransa Romain Folz na Msaidizi wake, Mspaniola Alejandro Manu Rodríguez Lázaro, Kocha wa Makipa, Majdi Mnasria na Mtaalamu wa Viungo (Physiotherapist), Youssef Ammar wote kutoka Tunisia.
Wataalamu wengine wa Benchi la Ufundi ni Kocha wa Physic, Tshephang ‘Chyna’ Mokaila kutoka Botswana, Mchambuzi wa Video, Thula Bantu na Mkurugenzi wa Ufundi, Paul Matthews wote raia wa Afrika Kusini.








