HABARI ZA NYUMBANI
WAWILI WAJITOKEZA KUWANIA UENYEKTI BODI YA LIGI DHIDI YA RAIS WA AZAM FC

KAIMU Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Nassor Idrisa Mohamed atachuana na Said Soud Said na Hoseah Hopaje Lugano katika kuwania Uenyekiti wa TBLP.
Wagombea hao watatu, Father ambaye ni Rais wa Azam FC, Soud wa Coastal Union lakini anaingia kama Mwenyekiti wa Mtibwa Sugar na Lugano wa Namungo pamoja na wengine wote wa nafasi nyingine wanatakiwa kufika kwenye Usaili utakaofanyika OKtoba 15 Jijini Dar es Salaam.





