“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA ZAMBIA NYUMBANI KUFUZU KOMBE LA DUNIA

WENYEJI, Tanzania ‘Taifa Stars’ wamechapwa bao 1-0 na Zambia ‘Chipolopolo’ katika mchezo wa mwisho wa Kundi E Kufuzu Kombe la Dunia 2026 usiku wa Jumatano Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Bao pekee la Zambia leo limefungwa na mshambuliaji wa Al-Fayha ya Saudi Arabia, Junior Fashion Sakala akimtungua kipa mpya wa Simba SC ya nyumbani dakika ya 75.
Ni kipigo cha pili mfululizo nyumbani ndani ya mwezi mmoja kufuatia kuchapwa 1-0 tena na Nigeria katika mchezo mwingine wa Kundi E kufuzu Kimbe la Dunia Septemba 9 hapo hapo Uwanja wa Amaan.
Kwa matokeo hayo, Zambia inafikisha pointi tisa ingawa kuelekea mchezo wake wa mwisho wa Kundi hilo dhidi ya Niger Oktoba 12 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola, wakati Tanzania inakamilisha mechi zake za kundi hilo ikiwa na pointi 10 katika nafasi ya nne.
Niger ambayo jana imeichapa Kongo-Brazzaville mabao 3-1 Uwanja wa Agosti 4 Jijini Ouagadougou nchini Burkina Faso inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya pili.

Tayari Morocco imekwishafuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Canada, Mexico na Marekani baada ya kujihakikishia uongozi wa Kundi E.
Niger na Zambia zinawania kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo ili ziende kwenye mchujo wa kuwania nafasi ya ziada ya kufuzu michuano hiyo.
Timu tisa zitakazoongoza makundi zitafuzu moja kwa moja kuiwakilisha kwenye Fainali za Kombe la Dunia, wakati washindi wa pili bora wanne wa makundi watamenyana katika Nusu Fainali na Fainali na mshindi atakwenda kushiriki mchujo wa Mabara kuwania nafasi ya kwenda Kombe la Dunia pia.
Mchujo wa Mabara, unaojulikana kama Inter-Confederation Play-Offs ni michuano mingine midogo inayoshirikisha timu sita za Mabara manne duniani, kasoro UEFA kutafuta timu mbili za mwisho za kushiriki michuano hiyo.
Kutokana na Eritrea kujitoa katika Kundi E kabla ya kucheza mechi hata moja — FIFA imesema timu za makundi mengine nane zitakazomaliza nafasi ya pili zitapokonywa pointi zilizovuna kwenye dhidi ya timu zilizoshika mkia ili kujenga uwiano sawa katika kufuzu kwenye mchujo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button