SIMBA YACHAPWA 4-1 NA AL HILAL MECHI YA KIRAFIKI BUNJU

TIMU ya Simba SC imechapwa mabao 4-1 na Al Hilal Omdurman katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Gymkhana Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Al Hilal yamefungwa na winga raia wa Mali, Adama Coulibaly mawili, kiungo Msenegal, Madické Kane na mshambuliaji Mnigeria, Sunday Damilare Adetunji wakati la Simba amefunga winga Mkongo, Elie Mpanzu Kibisawala.
Ulikuwa mchezo wa pili ndani ya siku tatu baada ya Simba SC kuibuka na ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa kirafiki hapo hapo Mo
Simba Arena.
Mchezo huo ulikuwa maalum kwa timu zote kujiandaa na mechi zao za kwanza za Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi ijayo, Al Hilal wakiwa wageni wa Polisi ya Kenya Uwanja wa Taifa wa Nyayo Jijini Nairobi nchini Kenya na Simba SC wakiwafuata Nsingizini Hotspurs Uwanja wa Taifa wa Somhlolo mjini Lobamba nchiji Eswatini.



