“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

SIMBA SC YAREJEA DAR, KUCHEZA NA GOR MAHIA SIMBA DAY

KIKOSI cha Simba kimerejea Dar es Salaam Alfajiri ya leo baada ya kambi takriban mwezi mmoja nchini Misri kujiandaa na msimu mpya.
Mara baada ya kuwasili kikosi hicho kimeelekea moja kwa moja kambini Mbweni na kesho kitaanza tena mazoezi Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju.
Simba itacheza na vigogo wa Kenya, Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki kwenye tamasha la Simba Day Septemba 10 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Baada ya hapo Simba watarejea tena Uwanja wa Mkapa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Yanga Septemba 16.
Ikiwa nchini Misri, Simba imepata mechi tano za kujipima ikishinda tatu, kufungwa moja na kutoa sare moja.
Ilishinda 2-0 dhidi ya wenyeji, Wadi Degla ya Ligi Kuu ya nchini humo, 1-0 dhidi ya Al Zulfi inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia na 2-0 dhidi ya Carabat FC inayoshiriki Ligi ya Kanda nchini Misri.
Mechi nyingine nyingine ilifungwa 4-3 na ENPPI ya Ligi Kuu ya Misri Jijini Cairo na kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na FC Fassell ya Liberia.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button