“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

SIMBA SC YAICHAPA WADI DEGLA 2-0 CAIRO

TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wadi Degla SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri katika mchezo wa kirafiki leo Jijini Cairo.
Mabao ya Simba SC katika mchezo wa leo yamefungwa na viungo washambuliaji, Kibu Denis Prosper na Mkongo, Elie Mpanzu Kibisawala huo ukiwa mchezo wa nne katika kambi ya timu hiyo kujiandaa na msimu mpya nchini Misri.
Katika mechi tatu za awali kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Misri — Simba ilishinda mbili na kufungwa moja.


Ilishinda 1-0 Jijini Cairo dhidi ya Al Zulfi inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia na 2-0 Jijini Ismailia dhidi ya Carabat FC inayoshiriki Ligi ya Kanda nchini Misri, wakati mechi nyingine ilifungwa 4-3 na ENPPI ya Ligi Kuu ya Misri Jijini Cairo.
Simba SC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini kesho inatarajiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Liberia, FC Fassell.
Baada ya hapo Simba SC itarejea nchini tayari kwa tamasha lake la kutambulisha kikosi cha msimu mpya, Simba Day Septemba 10 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Baada ya Simba Day watarudi Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao, Yanga Septemba 16.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button