“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

SIMBA SC YAICHAPA AL HILAL 2-1 MECHI YA KIRAFIKI DAR

TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua kipindi cha kwanza na mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah la ushindi kipindi cha pili, wakati Al Hilal lilefungwa na winga raia wa Mali, Adama Coulibaly.
Mchezo huo ulikuwa maalum kwa timu zote kujiandaa na mechi zao za kwanza za Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi ijayo, Al Hilal wakiwa wageni wa Polisi ya Kenya Uwanja wa Taifa wa Nyayo Jijini Nairobi nchini Kenya na Simba SC wakiwafuata Nsingizini Hotspurs Uwanja wa Taifa wa Somhlolo mjini Lobamba nchiji Eswatini.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button