HABARI ZA NYUMBANI
ROMAIN FOLZ ANAENDELEA NA KAZI YANGA SC KWA AMANI KABISA

KOCHA Mfaransa, Romain Folz leo ameongoza mazoezi ya Yanga SC na kuzima uvumi kwamba klabu hiyo inataka kuachana naye baada ya miezi miwili tu kazini.
Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya mwishoni mwa wiki baada ya sare ya bila mabao na Mbeya City Septemba 29 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Na leo wamerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers Oktoba 18 Uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini Malawi, kabla ya timu hizo kurudiana Oktoba 25 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.




