“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

PATRICK MABEDI KOCHA MPYA MSAIDIZI YANGA SC

BEKI wa zamani wa Kimataifa wa Malawi, Patrick Mabedi (52) ametbulishwa kuwa kocha mpya Msaidizi wa Yanga — na amekaribishwa vizuri na Kocha Mkuu wa sasa, Mfaransa, Romain Folz.
Patrick Mabedi ambaye enzi zake anachezea timu ya taifa ya Malawi alipewa jina la utani, Bosti au The General amejiunga na kikosi cha Yanga leo mazoezini na anatarajiwa kuanza kazi mara moja.
Enzi zake amechezea klabu za Big Bullets kuanzia mwaka 1997 hadi 1998 alipohamia Afrika Kusini na kuchezea Kaizer Chiefs hadi 2006 akajiunga na Moroka Swallows hadi 2008 alipostaafu soka na kuanza mafunzo ya Ukocha.

Alianza kama Kocha Msaidizi wa Moroka Swallows kati ya 2014 na 2015 alipohamia Black Aces hadi 2016 akarejea nyumbani kuwa kocha Msaidizi wa timu yake ya taifa, Malawi.
Mwaka 2017 alikwenda tena Afrika Kusini ambako aliendelea na Ukocha Msaidizi wa klabu za Cape Town All Stars hadi 2018 akahamia Kaizer Chiefs ambako mwaka 2019 alipewa Ukocha wa Muda, kabla ya kuhamia Black Leopards baadaye mwaka huo kama Kocha Msaidizi pia.
Mwaka 2020 aliajiriwa kama Kocha Mkuu kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya vijana ya Malawi U20 hadi 2023 akapandishwa timu ya wakubwa alipofanya kazi hadi mwaka jana alipompisha Mzimbabwe, Kalisto Pasuwa.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button