“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
Uncategorized

OPA CLEMENT AJIUNGA NA TIMU YA LIGI KUU HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa kike wa Kimataifa wa Tanzania, Opah Clement Tukumbuke (24) amejiunga na klabu ya SD Eibar ya Ligi Kuu ya Hispania akitokea FC Juárez ya Mexico.
Opa anajiunga na SD Eibar baada ya kuichezea FC Juárez kwa nusu msimu kufuatia kujiunga nayo Februari 2, mwaka huu akitokea Henan FC ya China.
Opa ni mchezaji aliyeibukia katika sekondari ya Makongo mwaka 2019, kabla ya kusajiliwa na Evergreen alikocheza kwa msimu mmoja kabla ya kwenda Kigoma kuchezea Kigoma Sisters kwa msimu mmoja pia.
Mwaka 2021 alijiunga na Simba Queens na baada ya kufanya vizuri anajiunga na Kayseri Kadin FK ya Uturuki kwa mkopo kwa nusu msimu akarejea Msimbazi.
Machi 5, mwaka 2023 alijiunga na Beşiktaş ya Uturuki hadi Julai 24 mwaka 2024 alipokwenda Henan FC ya China.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button