“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

NI JKT QUEENS WASHINDI NGAO YA JAMII WANAWAKE 2025

TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba Queens katika mchezo wa Fainali ya michuano ya timu nne jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Queens yamefungwa na Winfrida Gerard Hubert dakika ya 12 na beki wa kushoto, Asha Omary Ramadhan aliyejifunga dakika ya 17, wakati la Simba Queens limefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Zawadi Usanase Umukinnyi dakika ya 90’+5.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Yanga Princess iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mashujaa Queens hapo hapo KMC Complex.
Mabao ya Yanga Princess yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Jeannine Mukandayisenga dakika ya 16 na viungo, Mnigeria Precious Christopher dakika ya 48 na Muhabeshi, Aregash Kalsa dakika ya 65.
Wakati Mashujaa Queens ikifungwa 2-0 na Simba Queens katika mechi za Nusu Fainali, Yanga Princess ilitolewa na JKT Queens kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 1-1 hapo hapo KMC Complex.

Pamoja na kutwaa Ngao ya Jamii Wanawake — JKT Queens pia imetoa Mchezaji Bora, Winfrida Gerard Hubert na Kipa Bora, Naijat Abbas wakati mshambuliaji Mnyarwanda wa Yanga, Jeannine Mukandayisenga ‘Kaboy’ amekuwa Mfungaji Bora.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button