“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI MOTOMOTOHABARI ZA KIMATAIFAHABARI ZA ULAYA

NI CHELSEA BINGWA WA DUNIA 2025, PSG YAPIGWA 3-0 MAREKANI

TIMU ya Chelsea ya England imefanikiwa kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa usiku huu Uwanja wa MetLife, East Rutherford, Bergen County, New Jersey, Marekani.
Pongezi kwa kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa England, Cole Jermaine Palmer aliyefunga mabao mawili dakika ya 22 na 30, mshambuliaji mpya, Mbrazil João Pedro Junqueira de Jesus maarufu tu kama João Pedro kufunga la tatu dakika ya 43.

Kipindi cha pili Paris Saint-Germain walijaribu kusawazisha mabao bila mafanikio, huku Chelsea bao wakipoteza nafasi za kuongeza mabao walizotengeza.
Paris Saint-Germain walipata pigo dakika ya 85 baada ya kiungo wao ambaye hucheza beki ya kulia pia, João Pedro Gonçalves Neves kutolewa kwa kadi nyekundu.
Mchezo huo ulihudhuriwa na Rais wa Marekani, Donald Trump aliyekuwa Meza Kuu na Rais wa FIFA, Gianni Infantino na kukabidhi taji kwa Chelsea.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button