“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

MZIZE AFANYIWA UPASUAJI WA GOTI TAKUWA NJE KWA MIEZI MITATU

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga, Clement Francis Mzize atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki nane hadi 10 baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ally Shaaban Kamwe amesema kwamba Mzize amefanyiwa upasuaji kwa ushauri wa jopo la madaktari wakishirikiana na benchi la Ufundi na Mchezaji mwenyewe tulikubali juu ya hilo.
“Maamuzi haya yalikuja baada ya kuona anaendelea kupata maumivu kwenye goti lake kila alipokuwa akirejea uwanjani. Nipende kuutangazia Umma kuwa, mchezaji Clement Mzize atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nane mpaka kumi,” amesema Kamwe.

Mzize aliumia katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Wiliete Septemba 19 Yanga ikishinda 3-0 Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda nchini Angola.
Aidha, Kamwe amesema kikosi cha Yanga kilirejea kambini jana kuanza maandalizi ya mchezo wake wa Jumapili wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya KMC Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Kuhusu mchezo wetu dhidi ya Prisons SC uliyopangwa kuchezwa Dodoma kabla ya kuahirishwa kwa angalizo la Kiusalana, Kamwe amesema kwamba wanasubiri tarehe mpya itakayopangwa na Bodi ya Ligi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button