“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

MWANDISHI WA HABARI WA ETHIOPIA AWA KOCHA MSAIDIZI AZAM FC

KLABU ya Azam FC imemtambulisha Mhabeshi, Addis Worku kuwa Kocha wake Msaidizi akitokea Al Hilal ya Sudan ambako alikuwa Kocha Msaidizi na Mchambuzi wa kiwango cha mchezo.
Worku aliachia ngazi klabu hiyo yenye maskani yake Omdurman Juni mwaka huu kabla ya kuanza kwa Ligi ya mpya ya Sudan akifuata nyayo za aliyekuwa bosi wake, Mkongo Florent Ibenge ambaye pia amejiunga na Azam FC mapema mwezi huu.
Worku alitakiwa kujiunga na Fasil Kenema ya Ligi Kuu ya kwao, Ethiopia ambayo ilimtengea mkataba wa miaka mitano, lakini hakutaka kwenda kuchukua nafasi ya Wubetu Abate ambayo klabu hiyo inataka kuachana naye.

Mzaliwa huyo wa Addis Ababa, Worku ni mpenda mbinu za soka ambaye aliibuka kwa mara ya kwanza kama mwandishi wa gazeti la kila wiki la Ethiopia linaloitwa Ethio Sport.
Uamuzi wake ulimsaidia kuwa mchambuzi wa video na kupata leseni yake ya ukocha huko Ireland. Anasifiwa kwa kuisaidia Saint George kutwaa mataji mfululizo ya ligi ya Ethiopia mwaka wa 2022 na 2023 akiwa chini ya Kocha Mkuu Zerihun Shengeta.
Worku pia amefanya kazi kama mchambuzi wa video katika timu za taifa za Uganda na Zambia chini ya Kocha Mserbia, Micho Sredoje

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button