“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

MTANZANIA ASHINDA MEDALI YA SHABA CHICAGO MARATHON

MWANARIADHA shupavu wa Tanzania, Magdalena Crispine Shauri ametikisa ulimwengu kwa kuibuka na Medali ya Shaba katika mashindano ya kifahari ya Chicago Marathon 2025 huko Marekani.
Magdalena amekimbia kwa muda wa kihistoria wa Saa 2:18:03 (PB – Personal Best), akivunja Rekodi ya Taifa ya Tanzania kwa mbio ndefu (Marathon) kwa wanawake.
Amezidiwa na wakimbiaji wawili wa Ethiopia, Hawi Feysa aliyeongoza akitumia muda wa Saa 2:14:56 na kushinda Medali ya Dhahabu na Megertu Alemu aliyetumia muda wa Saa 2:17:18 na kushinda Medali ya Fedha.

Hii si mara ya kwanza kwa Magdalena Shauri kushinda Medali, kwani Septemba 24, 2023 alishinda tena Medali ya Shaba kwa kushika nafasi ya 3 kwa muda wa 2:18:41 kwenye Berlin Marathon nchini Ujerumani.
Magdalena Shauri ni mfano wa kuigwa, ishara ya Nguvu, Kasi, na Uzalendo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button