“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKA

MOROCCO YAITOA SENEGAL KWA MATUTA, YAINGIA FAINALI CHAN

TIMU ya Morocco imefanikiwa kwenda Fainaliya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa penalti 5-3 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 na Senegal usiku wa Jumanne Uwanja wa Taifa waMandela Jijini Kampala, Uganda.
Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua wa Nusu Fainali, beki wa kushoto wa Teungueth FC, Layousse Samb alianza kuifungia Senegal dakika ya 16, kabla ya kiungo wa Raja Athletics, Sabir Bougrine kuisawazishia Morocco dakika ya 23.

Kwenye mikwaju ya penalti waliofunga za Morocco ni Hrimat, Lamlioui, Bach na Mehri huku Khairi pekee akikosa.
Upande wa Senegal waliofunga ni Vieux, Ciss na Ba baada ya Ndiaye kukosa ya kwanza.
Morocco sasa itakutana na Madagascar katika Fainali Jumamosi ya Agosti 30 Uwanja wa Moi International Sports Centre, Nairobi — wakati Senegal itakutana tena na wapinzani wao wa Kundi C, Sudan katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Ijumaa ya Agosti 29 Uwanja wa Mandela, Kampala.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button