“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

MCHEZO WA TAIFA STARS NA SENEGAL MICHUANO YA CECAFA WASOGEZWA MBELE

MCHEZO kati ya wenyeji, Tanzania na Senegal wa michuano maalum ya mataifa manne inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) umesogezwa mbele hadi Julai 27.
Taarifa ya CECAFA jioni ya leo imesema kwamba sababu za kusogezwa mbele kwa mchezo huo na taratibu za kuwasili kwa Senegal ambao watachelewa, hivyo kutokuwa tayari kwa mchezo wa kesho Saa 10:00.
Lakini kwa ujumla michuano hiyo itaanza kesho kama ilivyopangwa Uwanja wa Karatu Jijini Arusha ila kutakuwa na mchezo mmoja tu kati ya Kenya ‘Harambee Stars’ na wenyeji, Tanzania ‘Taifa Stars’ Saa 10:00 jioni.
Mechi za pili zitafuatia Alhamisi ya Julai 24 hapo hapo Uwanja wa Karatu, kwa Uganda kumenyana na Kenya Saa 7:00 mchana, kabla ya Tanzania kucheza na Senegal.
Mechi za mwisho zitafuatia Julai 27 kwa mahasimu Kenya na Uganda Saa 7:00 mchana kabla ya Tanzania kumenyana na Senegal 10:00 Jioni.

Senegal celebrates victory with trophy during 2022 CAF African Nations Championship Final football match between Algeria and Senegal at the Nelson Mandela Stadium in Algiers, Algeria on 04 February 2023 ©Gavin Barker/BackpagePix

Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, Mkenya John Auka Gecheo michuano hiyo ni fursa nzuri ya maandalizi kwa timu za ukanda wake, Kenya na Uganda na Tanzania kupata maandalizi ya mwisho kabla ya Fainali za Kombe la Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
Fainali za CHAN zinatarajiwa kuanza Agosti 2 hadi 30, mwaka huu zikiwa zinaandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Kenya, Tanzania na Uganda.
Katika CHAN Kundi A kuna Kenya, Morocco, Angola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia, Kundi B kuna Tanznaia, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), wakati Kundi C linazikutanisha Uganda, Niger, Guinea, Algeria na Afrika Kusini wakati Kundi D kuna Senegal, Kongo, Sudan na Nigeria.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button