HABARI ZA AFRIKA
MAYELE APIGA ZOTE, PYRAMIDS YAICHAPA APR 2-0 KIGALI

MSHAMBULIAJI wa Pyramids, Fiston Kalala Mayele akimpa jezi mchezaji mchezaji mwenzake wa zamani wa AS Vita ya kwao, DRC na Yanga ya Tanzania, Jesus Moloko baada ya mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, APR leo Uwanja wa Pele, Nyamirambo Jijini Kigali nchini Rwanda.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika wameshinda 2-0, mabao yote yakifungwa na Mayele dakika ya 49 na 86.
Timu hizo zitarudiana Oktoba 5 Uwanja wa Juni 30 Jijini Cairo na mshindi wa jumla atakutana na Ethiopian Insurance ya Ethiopia Ethiopia ambayo imeitoa Mlandege SC ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 4-3 ikishinda 2-0 nyumbani na kufungwa 3-2 ugenini.






