“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AFRIKA

MAMELODI SUNDOWNS WATUA MAREKANI NA WACHEZAJI 26 KLABU BINGWA YA DUNIA FIFA

MABINGWA wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns wametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaokwenda nao Marekani kwenye michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA inayotarajiwa kuanza Jumamosi ijayo, Juni 14 hadi Julai 13, 2025.
Sundowns, ambayo inajulikana kwa jina la utani Kama Masandawana wataanza kampeni yao kwa kumenyana na vigogo wa Japan, Ulsan Jumanne, Juni 17 Uwanja wa Inter&Co. Jijini Orlando, Florida, kabla ya kucheza na Borussia Dortmund ya Ujerumani
Jumamosi ya Juni 21 Uwanja wa TQL mjini Cincinnati na kukamilisha mechi zao za Kundi F Juni 25 Uwanja wa Hard Rock, Miami Gardens.
Msafara wa Sundowns unaohusisha wachezaji 26, Kocha Mkuu Miguel Cardoso, viongozi na Maafisa wengine uliondoka juzi Jumapili na umewasili salama Marekani tayari kwa michuano.
Kikosi kilichoondoka kinaundwa na makipa: Ronwen Williams, Denis Onganyo na Reyaad Pieterse
Mabeki: Khuliso Mudau, Thapelo Morena, Aubrey Modiba, Divine Lunga, Grant Kekana, Malibongwe Khoza, Mothobi Mvala, Keanu Cupido na Mosa Lebusa
Viungo: Marcelo Allende, Jayden Adams, Themba Zwane, Sphelele Mkhulise, Neo Maema, Teboho Mokoena na Bathusi Aubaas
Washambuliaji: Peter Shalulile, Lucas Ribeiro Costa, Iqraam Rayners, Arthur Sales, Tashreeq Matthews, Lebo Mothiba na Kutlwano Letlhaku.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button