“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

LIGI KUU KUREJEA JUMAMOSI, SIMBA NA JKT TANZANIA KUMENYANA MEJA ISAMUHYO

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesema kwamba Ligi Kuu ya NBC na Ligi ya Championship Tanzania zote zinarejea baada ya kusimama kwa muda tangu Oktoba 29 kwa angalizo la Kiusalama.
Taarifa ya TPLB imesema mechi za Ligi Kuu na Championship zitaendelea kuanzia Jumamosi ya Novemba 8 siku ambayo Pamba Jiji watawakaribisha Singida Black Stars kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Simba SC kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Na Jumapili ta Novemba 9, mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa wenyeji wa KMC kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam – kabla ya Namungo FC kucheza na Azam FC kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button