INTER MILAN NA MONTERREY ZASONGA MBELE KOMBE KA DUNIA

TIMU ya Inter Milan ya Italia imefanikiwa kwenda Hatua ya Mtoa ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya River Plate ya Argentina katika mchezo wa Kundi E Alfajir ya leo Uwanja wa Lumen Field, Seattle, Washington, Marekani.
Mabao ya Inter Milan yamefungwa na Wataliano ote, mshambuliaji, Francesco Pio Esposito dakika ya 72 na beki wa kati, Alessandro Bastoni Cavaliere dakika ya 90’+3.
Mechi nyingine ya Kundi E Alfajiri ya leo, CF Monterrey ya Mexico imeichapa Urawa Red Diamonds ya Japan 4-0 mabao ya
Nelson Deossa dakika ya 30, Germán Berterame mawili, dakika ya 34 na 90’+7 na Jesus Manuel Corona dakika ya 39 Uwanja wa Rose Bowl, Pasadena, California.
Kwa matoke ohayo, Inter Milan inamaliza na pointi sana kileleni mwa Kundi G ikifuatiwa na CF Monterrey iliyomaliza na pointi tano, wakati River Plate imeondoka na pointi nne huku Urawa wanaondoka mikono mitupu baada ya kufungwa mechi zote tatu.




