“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AMERIKAHABARI ZA KIMATAIFAHABARI ZA ULAYA

GUIRASSY AIPELEKA BORUSSIA DORTMUND ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

TIMU ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Monterrey ya Mexico Alfajiry ya leo Uwanja wa Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia, Marekani.
Mabao yote ya Borussia Dortmund yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Guinea, Serhou Yadaly Guirassy mzaliwa wa Ufaransa dakika ya 14 na 24, wakati bao pekee la mshambuliaji Kimataifa wa Mexico, Germán Berterame mzaliwa wa Argentina dakika ya 48.
Sasa Borussia Dortmund itakutana na Real Madrid ya Hispania ambayo imeitoa Juventus ya Italia usiku wa jana kwa kuichapa bao 1-0 Uwanja wa Hard Rock, Miami Gardens, Dade County, Florida, Marekani.
Bao pekee la Real Madrid limefungwa na mshambuliaji chipukizi wa umri wa miaka 21, Gonzalo García Torres zao la timu ya vijana ya klabu hiyo dakika ya 54 akializia krosi ya beki mpya, Muingereza Trent Alexander-Arnold dakika ya 54.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button