“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

FOUNTAIN GATE YAZINDUKA, YAICHAPA DODOMA JIJI YAICHAPA 1-0 BABATI

TIMU ya Fountain Gate imepata ushindi wa kwanza wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuichapa 1-0 Dodoma Jiji katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mudrick Abdi Shehe dakika ya 90’+2 huo ukiwa ushindi wa kwanza katika mechi nne, nyingine zote tatu za awali ikifungwa 2-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, 3-0 na Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa, dar es Salaam na 1-0 dhidi ya Mbeya City hapo hapo wa Tanzanite Kwaraa.
Kwa upande wao, Dodoma Jiji baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao nne katika mechi nne kufuatia kushinda mechi moja, 2-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Jamhuri, Dodoma sare ya 2-2 na TRA United Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora na kufungwa 1-0 na KMC Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button