ESPÉRANCE YAANZA VIBAYA KOMBE LA DUNIA, YACHAPWA 2-0 NA FLAMENGO

WAWAKILISHI wa Afrika, Espérance ya Tunisia wameanza vibaya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya kufungwa mabao 2-0 na Flamengo ya Brazil katika mchezo wa KUndi D usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Lincoln Financial Field, Philadelphia, Marekani.
Mabao ya Flamengo yamefungwa na mawinga wa Uruguay, De Arrascaeta dakika ya 17 na Luiz Araújo wa Brazil dakika ya 70 mbele ya mashabiki 25,797 waliojitokeza katika mechi iliyochezeshwa na refa Mholanzi, Danny Makkelie.
Mchezo mwingine wa Kundi D jana usiku Chelsea ya England ilianza vyema kwa ushindi wa 2–0 dhidi ya wenyeji, Los Angeles FC mabao ya winga Mreno, Neto dakika ya 34 na kiungo Muargentina, Enzo Fernández dakika ya 79 Uwanja wa Mercedes-Benz Stadium, Atlanta mechi iliyochezeshwa na refa Jesús Valenzuela wa Venezuela.
Mchezo wa Kundi C baadaye jana Boca Juniors ya Argentina ilitoka sare ya 2–2 na Benfica ya Ureno Uwanja wa Hard Rock, Miami Gardens.
Mabao ya Boca Juniors yalifungwa na Miguel Merentiel wa Uruguya dakika ya 21 na beki Muargentina, Rodrigo Battaglia dakika ya 27, wakati ya Benfixa yalifungwa na Wareno, winga beki Angel Di María kwa penalti dakika ya 45’+3 na Nicolas Otamendi dakika ya 84 mbele ya mashabiki 55,574 mechi iliyochezeshwa na refa César Ramos wa Mexico.




