“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

DIARRA MCHEZAJI BORA WA KWANZA WA MSIMU LIGI KUU, AHMAD ALI KOCHA BORA

KIPA wa Yanga SC, Djigui Diarra raia wa Mali ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi wa kwanza wa msimu, Septemba 2025, huko Ahmad Ally wa JKT Tanzania akibeba Tuzo ya Kocha Bora kwa mwezi huo.
Diarra amenyakua Tuzo akiwaangusha beki Muivory Coast, Anthony Urbain Tra Bi Tra wa Singida Black Stars na kiungo wa JKT Tanzania, Mohamed Bakari – wakati Ally ameshinda Tuzo hiyo dhidi ya Mfaransa Romain Folz wa Yanga na Muargentina, Miguel Gamondi wa Singida Black Stars.
Diarra amedaka mechi mbili za Ligi Kuu bila kuruhusu bao, akionyesha uhodari mkubwa kwenye mechi zote hizo kwa kuokoa michomo mingi ya hatari Yanga ikishinda 3-0 dhidi ya Pamba Jiji FC Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kutoa sare ya bila mabao na wenyeji, Mbeya City Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Ally ameiongoza JKT Tanzania kukusanya pointi tano katika mechi tatu, mbili za ugenini akishinda 2-1 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na sare ya 1-1 na Mashujaa Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma na nyingine ya 1-1 nyumbani na Azam FC Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button