“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

CHIPUKIZI MTANZANIA ASAJILIWA KLABU YA LIGI KUU SWEDEN

KIUNGO mshambuliaji Chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Sabri Dahary Kondo (19) amejiunga na BK Häcken FF ya Ligi Kuu ya Sweden kwa mkataba wa miaka minne akitokea Singida Black Stars.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, BK Häcken FF imesema Kondo mchezaji mwenye kipaji adhimu kutoka Tanzania amejiunga nao kwa mkataba ambao utafikia tamati mwaka 2029.
Kondo alijiunga na Singida Black Stars katika dirisha dogo Januari mwaka huu akitokea KVZ ya Zanzibar, lakini akatolewa kwa mkopo Coastal Union ya Tanga.

Chipukizi huyo alikuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichotwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, CECAFA U20 Oktoba mwaka jana nchini akiibukia mfungaji wa michuno hiyo.
Chipukizi huyo alikuwepo pia kwenye kikosi hicho cha Ngorongoro Heroes kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) U20 nchini Misri.
Juni mwaka huu Kondo alishinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora Chipukizi wa mwaka 2024 Tanzania katika Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button