“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA NYUMBANI

AZAM FC YAPANGWA NA WYDAD, SINGIDA NA BELOUIZDAD MAKUNDI SHIRIKISHO

TIMU ya Azam FC imepangwa Kundi B katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na Wydad Casablanca ya Morocco, AS Maniema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Nairobi United ya Kenya.
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, Singida Black Stars wamepangwa Kundi C pamoja na CR Belouizdad ya Algeria, Stellenbosch FC ya Afrika Kusini na AS Otoho Kongo-Brazzaville.
Kundi linazikutanisha USM Alger ya Algeria, Djoliba AC de Bamako ya Mali, Olympique Club de Safi ya Morocco na FC San Pedro ya Ivory Coast, wakati Kundi D kuna Zamalek, Al Masry zote za Misri, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na ZESCO United ya Zambia.

RATIBA MECHI ZA MAKUNDI
KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Mechi za Kwanza: 21-23 November
Mechi za Pili: 28-30 November
Mechi za Tatu: 23-25 January
Mechi za Nne: 30 Janunary-01 February
Mechi za Tano: 06-08 February
Mechi za Sita: 13-15 February

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button