HABARI ZA NYUMBANI
AZAM FC YAMSAJILI LAMECK LAWI WA COASTAL UNION

KLABU ya Azam FC imeanza kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao baada ya usiku huu kumtambulisha beki Lameck Elias Lawi kuwa mchezaji wake wa kwanza mpya.
Beki huyo wa kati anajiunga na Azam FC baada ya misimu mitatu ya kufanya vyema akiwa na klabu ya Coastal Union ya Tanga hadi kuchaguliwa timu ya taifa ya vijana chini ya Umri wa miaka 20.

Beki huyo wa kati aliyezaliwa Septemba 12, mwaka 2005 Jijini Arusha aliiongoza U-20 ya Tanzania Ngorongoro Heroes’ kutwaa ubingwa wa CECAFA mwaka jana na kupata tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON U20) mapema mwaka huu.




