HABARI ZA NYUMBANI
AZAM FC YAICHAPA APR 2-0 AMAHORO

TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, APR katika mchezo wa kirafiki wa michuano hiyo maalum iliyoandaliwa na wenyeji wa hao.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali, mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo washambuliaji, Zidane Sereri dakika ya 45’+2 na Yahya Zayd dakika ya 54.
Ulikuwa mchezo wa tatu kwa Azam FC kwenye michuano hiyo ya ‘APR Better Pre Season’ baada ya awali kuifunga Polisi kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 na kufungwa 2-1 na AS Kigali katika mechi zote zikipigwa Uwanja wa Pele, Nyamirambo.




