HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIHABARI ZA NYUMBANI
AZAM FC YACHAPWA 1-0 NA AS KIGALI NYAMIRAMBO

TIMU ya Azam FC leo jioni ya leo imefungwa bao 1-0 na wenyeji, AS Kigali katika mchezo wa pili wa michuano ya ‘Better APR FC Pre Season Tournament’ Uwanja wa Pele, Nyamirambo, Kigali nchini Rwanda.
Bao pekee la AS Kigali limefungwa na mshambuliaji chipukizi wa miaka 21 wa Kimataifa wa Rwanda, Prince Rudasingwa dakika ya 43 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye boksi na kipa Hamisi Yassin.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza Azam ilishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya wenyeji wengine, Polisi FC kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 hapo hapo Nyamirambo.
Azam FC watakamilisha mechi zao za michuano hiyo kwa kumenyana na wenyeji wengine na wenye michuano yao, APR FC hapo hapo Nyamirambo.




