“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI MOTOMOTOHABARI ZA NYUMBANI

AZAM FC YAACHANA KWA KHERI NA GIBRIL SILLAH

KLABU ya Azam FC imetangaza kuachana na winga wake Mgambia, Gibril Sillah (26) baada ya misimu miwili ya kuwa na timu hiyo kwa misimu miwili na nusu.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Azam FC imemuaga na kumshukuru Sillah ambaye naye pia kwenye kurasa zake amefanya hivyo.
Kwa mujibu wa Azam FC, katika kipindi cha misimu miwili na nusu, Sillah amecheza jumla ya mechi 68 akifunga mabao 21 na kutoa pasi za mabao 10 yaliyofungwa na wengine.


Sillah ameandika kuishukuru Azam FC akisema; “Asanteni Azam Football Club kwa yote mliyonifanyia katika kipindi hiki cha miaka miwili,”.
Sillah ameendelea; “Ni wakati mgumu kwangu kuiaga klabu, nina kumbukumbu nyingi nzuri ambazo sitoweza kuzisahau katika maisha yangu ya soka,”.
“Nawashukuru mashabiki wa klabu kwa muda wote mliokuwepo kwa ajili yangu katika wakati mzuri na mbaya, hakika nitaikosa sana klabu hii, lakini hayo ndiyo maisha, ninaitakia klabu mafanikio makubwa katika msimu ujao wa klabu,”ameandika.
Amewashukuru viongozi, makoch, Maafisa wengine wa benchi la Ufundi akiwemo mtunza vifaa na kuongeza;
“Na kila mtu ndani ya klabu kwa kunifanya kukaa ndani ya klabu, ilikuwa rahisi na kiukweli nitaikumbuka nchi hii kubwa Tanzania, sababu ni taifa la mpira wa miguu, kila mtu anapenda soka, ni kama unacheza Ulaya vibes huwa ni chanya 🙏Sitasahau kumbukumbu nzuri nchini na klabu yangu ya Azam FC itabaki moyoni mwangu daima naipenda klabu hii,”.


Sillah aliwasili Azam FC katika dirisha dogo Januari 7, mwaka 2023 akitokea Raja Casablanca ya Morocco baada ya awali kuchezea timu nyingine nchini humo, JS Soualem.
Alijiunga na Raja Agosti 27 mwaka 2021 akitokea Teungueth ya Senegal, lakini Januari 24 mwaka 2022 akapelekwa kwa mkopo JS Soualem alikocheza hadi anasajiliwa Azam FC.
Kabla ya kwenda Teungueth Julai 1, mwaka 2017 alichezea Samger FC na Fortune FC za kwao, Gambia.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button