HABARI ZA NYUMBANI
AZAM FC NA SINGIDA BLACK STARS WOTE KUANZIA UGENINI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika wote wataanzia ugenini – Azam FC ikienda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kumenyana na wenyeji, AS Maniema Union mechi za Kundi B Novemba 23, wakati Singida Black Stars watakwenda Algeria kumenyana na CR Belouizdad mechi ya Kundi C.








