FAINALI NBA 2025 NI FUNGA NIKUFUNGE; THUNDER 111-104 PACERS

TIMU ya Oklahoma City Thunder imetoka nyuma kwa pointi 10 kipindi cha pili na kishinda kwa pointi 111-104 dhidi ya Indiana Pacers Katika Game 4 ya Fainali za Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Gainbridge Fieldhouse Jijini Indianapolis.
Ilikuwa ni kazi nzuri ya Shai Gilgeous-Alexander aliyefunga pointi 15 kati ya zote 35 kwenye dakika 4:38 za mwisho kuipa Oklahoma City Thunder ushindi huo wa 111-104 na sasa wanalingana na Indiana Pacers kwa ushindi wa Series mbili kila timu.
Wengine waliotoa mchango mzuri kwenye ushindi huo ni Jalen Williams aliyefunga pointi 27, Alex Caruso pointi 20 na Chet Holmgren pointi 14 na rebounds 15.
Kwa upande wao Indiana Pacers waliofunga pointi nyingi ni Pascal Siakam 20, Tyrese Haliburton 18 na Obi Toppin 17.
Sasa tunakwenda kwenye Game 5 ya Series — tukirejea ukumbi wa Paycom Center Jijini Oklahoma City, Oklahoma Jumatatu usiku.
Ikumbukwe Game 1 Indiana Pacers ilishinda 111-110, Game 2 Oklahoma City Thunder ilishinda 123-107 na Game 3 Indiana Pacers ilishinda 116-107.