“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AMERIKA

INDIANA PACERS YAICHAPA THUNDER 116-107 GAME 3 FAINALI NBA 2025

WENYEJI, Indiana Pacers wameibuka na ushindi wa pointi 116-107 dhidi ya Oklahoma City Thunder katika Game 3 ya Fainali za Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani, NBA 2025 usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Gainbridge Fieldhouse Jijini Indianapolis.
Bennedict Mathurin alifunga pointi 27, Tyrese Haliburton akamaliza na pointi 22, assists 11 na rebounds tisa, wakati Pascal Siakam naye alifunga pointi 21 upande wa Pacers na sasa wanaongoza kwa Series 2-1.
Kwa upande wa Oklahoma City Thunder, Jalen Williams alifunga pointi 26, Shai Gilgeous-Alexander akaongeza 24 na Chet Holmgren akafunga 20 ingawa haikusaidia kuwapa ushindi licha ya kuingia quarter ya nne wakiwa wanaongoza kwa pointi tano.


Game 4 itafuatia Ijumaa kuamkia Jumamosi hapo Gainbridge Fieldhouse baada ya kila timu kushinda Game moja kati ya mbili zilizotangulia ukumbi wa Paycom Center Jijini Oklahoma City, Oklahoma.
Game 1 Indiana Pacers ilishinda 111-110 na Game 2 Oklahoma City Thunder ilishinda 123-107.
Mambo yatakuwaje Game 4? Ni jambo la kusubiri na kuona.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button