“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AMERIKA

OKLAHOMA CITY THUNDER YAIBAMIZA INDIANA PACERS 123-107 GAME 2 FAINALI NBA

TIMU ya Oklahoma City Thunder imeibuka na ushindi wa pointi 123-107 dhidi ya Indiana Pacers katika Game 2 ya Fainali za NBA 2025 usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Paycom Center Jijini Oklahoma City, Oklahoma.
Kwa ushindi huo, Oklahoma City Thunder wanasawazisha series na kuwa 1-1 kufuatia Indiana Pacers kushinda 111-110 katika Game 1 Alhamisi hapo hapo Paycom Center.
Nyota wa Oklahoma City Thunder leo ni Shai Gilgeous-Alexander baada ya MVP huyo wa NBA kufunga pointi 34 points, assists 8, rebounds 5 na steals 4.
Tyrese Haliburton alionyesha cheche zake kwenye quarter ya nne akifunga pointi 17, rebounds 3, assists 6 na turnovers 5, ingawa muda haukutosha kuokoa jahazi.
Mashabiki wa Pacers watatarajia kuona makali zaidi ya Haliburton katika Game 3 Jumatano wakiwa nyumbani ukumbi wa Gainbridge Fieldhouse Jijini Indianapolis.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button