“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI ZA AMERIKA

NI INDIANA PACERS NA OKLAHOMA CITY THUNDER FAINALI NBA 2025

FAINALI za NBA 2024-2025 itazikutanisha Indiana Pacers ya Western Conference na Oklahoma City Thunder ya Eastern.
Hiyo ni baada ya Pacers kuitoa New York Knicks usiku wa kuamkia leo kwa kuifunga pointi 125-108 kwenye Game 6 ya Fainali za Western Conference, hivyo kuingia Fainali za NBA 2024 kwa ushindi wa Series 4-2.
Pascal Siakam aliongoza kwa kufunga pointi nyingi, 31 katika mitupo 10 kati ya 18 akifanya pia rebounds tano na assists tatu, wakati Tyrese Haliburton alitamba katika quarter ya kwanza akifunga pointi 21 na assists 13.
Mchezaji aliyefanya vizuri Zaidi wa Pacers ni Andrew Nembhard, aliyefunga pointi 14, assists nane na steals sita.


Itakuwa Fainali ya kwanza ya NBA kwa Indiana Pacers Finals tangu mwaka 2000, wakati ambao ilikuwa inaundwa na nyota kama Reggie Miller na Jalen Rose chini ya Kocha Larry Bird.
Ikumbukwe kwa Eastern Conference Oklahoma City Thunder walikamilisha safari yao ya Fainali kwa ushindi wa pointi 124-94 dhidi ya Minnesota Timberwolves na kusonga mbele kwa ushindi wa Series 4-1.
Msimu uliopita Indiana Pacers walikwama mbele ya Boston Celtics baada ya kufungwa Series nne mfululizo, wakati Oklahoma City Thunder walitolewa katika Nusu Fainali na Dallas Mavericks kwa kufungwa Series 4-2.
Game 1 kati ya Pacers na Thunder itapigwa Alhamisi huko Oklahoma City, wakati Game 2 itafuatia Jumapili, Juni 8 huko huko Oklahoma City, huku Gainbridge Fieldhouse ikiwa mwenyeji wa Game 3 Jumatano ya Juni 11 na Game 4 itafuatia Ijumaa ya Juni 13.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button