“MARINE”    
“SAFINA”
“NGANO
“UNGA
“UNGA
“WATER”
HABARI MOTOMOTOHABARI ZA AFRIKA

BENHACHEM KOCHA MPYA WYDAD, YASAJILI MCHEZAJI WA HULL CITY

KLABU ya Wydad Athletic imemtambulisha Mmorrco Mohamed Amine Benhachem (49) kuwa kocha wake mpya, akichukua nafasi ya Rhulani Mokwena raia wa Afrika Kusini aliyeondoka mapema mwezi huu.
Benhachem ni kizazi kipya cha makocha wa Morocco anayeinukia vizuri, ambaye kama mchezaji wa nafasi ya ulinzi kwa miaka 10 kuanzia 1994 hadi 2004 akicheza klabu za Raja, RS Settat, HUS Agadir, Montreal Impact na Wydad AC zote za nyumbani, Royal WSB ya Ubelgiji na Ahli ya Dubai.
Amecheza pia timu ya taifa ya Morocco kati yam waka 2000 na 2001 kabla ya kuchezea timu ya taifa ya soka ya ufukweni kuanzia mwaka 2007 hadi 2008.
Amekuwa Kocha tangu mwaka 2008 alipostaafu akifundisha timu za CJ Houara, IR Tangier, RC Bernoussi, WA Fez, USM Aït-Melloul, AS Salé, OC Safi, OC Khouribga, SCC Mohammedia, FUS Rabat na RCA Zemamra zote za Morocco.
Pamoja na kocha huyo Wydad imetambulisha wachezaji wapya watatu ambao ni winga mkongwe Nourredine Amrabat kutoka Hull City ya England, mshambuliaji Hamza Hanouri kutoka FUS Rabat ya kwao na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stéphane Aziz Ki kutoka Yanga SC.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button