MABINGWA watetezi, Yanga watamenyana na Stand United katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati watani wao, Simba SC watamenyana na Mbeya City - vigogo wote wakipangiwa timu za Ligi ya Championship.
Robo Fainali nyingine za michuano hiyo iliyo katika mwaka wa pili wa udhamini wa Benki wa CRDB ni JKT Tanzania na Pamba Jiji Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam na Singida Black Stars dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Airtel mjini Singida.
Katika Nusu Fainali, Mshindi kati ya Yanga na Stand United atakutana na mshindi kati ya JKT Tanznaia Pamba Jiji na mshindi kati ya Simba SC na Mbeya City atakutana na mshindi kati ya Singida Black Stars na Kagera Sugar.
0 comments:
Post a Comment