RAIS wa klabu ya Yanga, Hersi Ally Said amesema kwamba mwaka ujao watajenga Uwanja wao kwa msaada wa Serikali.
Akizungumza kwenye Mkutano wa Viongozi wa Klabu Duniani ulioandaliwa na Taasisi ya World Football Summit (WFS) Jijini Rabat nchini Morocco, Hersi amesema kwamba klabu za Afrika zinakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombimu ikiwemo ukosefu wa viwanja vyao wenyewe.

Afrika tuna changamoto nyingi, mojawapo tumeitaja ni miundombinu . Tumeona Ulaya klabu nyingi zinamiliki miundombinu, ikiwemo vifaa vya mazoezi, vituo vya mafunzo, pamoja na viwanja vya kuchezea mechi, ambayo ni tofauti na klabu nyingi za Afrika,” amesema Hersi ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Klabu Afrika (ACA).
Ameongeza kwamba huwezi kuinua kipaji cha mchezaji kuwa cha kiwango bora bila ya kuwa na miundombinu na kuzipongeza baadhi ya klabu barani zenye miundombinu bora zikiwemo Al Ahly ya Misri.
“Kwa mfano klabu yangu, Yanga ni moja ya klabu kubwa ya umri wa miaka 90, lakini kusema ukweli hatuna Uwanja wetu wenyewe. Lakini uongozi wetu ndani ya mwaka mmoja ujao kwa msaada wa Serikali tutajenga Uwanja,”amesema Hersi.
Katika Mkutano huo, WFS ilimtunukia Tuzo Hersi kwa kazi yake nzuri ya kuziunganisha klabu barani Afrika akiwa Mwenyekiti wa ACA.
TAZAMA VIDEO RAIS WA YANGA AKIZUNGUMZA KWENYE MKUTANO WA WFS
0 comments:
Post a Comment