IMERIPOTIWA na kuthibitishwa, Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Ally Shaaban Kamwe alikamatwa jana baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Tabora United Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na kulala rumande.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha leo kwamba Jeshi hilo linamshikilia Kamwe tangu usiku wa jana alipokamatwa kwa tuhuma za kutoa lugha chafu kwa kwa viongozi wa Serikali.
Haya yote yalitokea baada ya mchezo wa jana ambao mabingwa watetezi, Yanga waliibuka na ushindi wa 3-0, mabao ya beki Israel Patrick Mwenda dakika ya 21 na washambuliaji Clement Francis Mzize dakika ya 57 na Mzimbabwe Prince Mpumelelo Dube dakika ya 68.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 61 katika mchezo wa 23 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya jirani zao, Simba ambao pia wana mechi moja mkononi – wakati Tabora United baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 37 za mechi 24 sasa nafasi ya tano.

Mchezo wa jana uliteka hisia za wengi, kwa sababu mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Tabora United iliifunga Yanga mabao 3-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Novemba 7, mwaka jana.
Ilikuwa siku nzito mno kwa Yanga ikifungwa mara ya pili mfululizo katika Ligi Kuu baada ya kuchapwa 1-0 na Azam FC Novemba 2 hapo hapo Azam Complex, bao pekee la winga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 33 akimalizia pası ya kiungo mzawa, Adolf Mtasingwa Bitegeko.
Mabao ya Tabora United pale Chamazi yalifungwa na winga mzawa, Offen Francis Chikola mawili dakika za 19 na 45’+4 mara zote akimalizia pasi za kiungo Mburkinabe, Yacouba Sogne na la tatu lilifungwa na kiungo Mkongo, Nelson Omba Munganga dakika ya 78 akimalizia pasi ya mshambuliaji mzawa, Ibrahim Ahmada ‘Hilika'.
Siku hiyo, nyota wa Yanga, Mburkinabe, Stephane Aziz Ki alikosa penalti iliyookolewa na kipa Hussein Masalanga kufuatia kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua kuangushwa kwenye boksi – na Yanga walipata bao la kufutia machozi dakika ya 90’+5, mfungaji Clement Francis Mzize akimalizia pasi ya mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo.
Kuelekea mchezo wa jana tambo na majigambo vilitawala kutoka kambi za timu zote mbili, zikiongozwa na Maafisa habari wa timu zote mbili, Kamwe na Christne Mwagala wa Tabora.
Mkuu wa Mkoa, Paul Matiko Chacha akazinogesha tambo hizo, ambazo wenyewe vijana wa sasa wanaziita ‘Amsha Amsha’ kwa kutangaza zawadi ya Sh. Milioni 60 kwa wachezaji wa Tabora United alipokutana nao mbele ya Waandishi wa Habari.
![]() |
Mkuu wa Mkoa, Paul Matiko Chacha alinogesha ‘Amsha Amsha’ za mechi ya Tabora United na Yanga kwa matamshi yake na ahadi ya Sh. Milioni 60 |
RC Chacha akakaririwa tena akisema amemsikia Afisa Habari wa Yanga, yaani Kamwe akitamba – lakini wao hawaihofii timu hiyo ya Jangwani, wanaiogopa timu moja tu nchi hii, Simba.
Chacha alisema hivyo kwa sababu msimu huu Simba imeifunga Tabora United mechi zote mbili za Ligi Kuu na zote 3-0, Agosti 18 Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam na Februari 2 Uwanja wa Mwinyi.
Lakini mbele ya Yanga ukiwazungumzia wao kwa kuwafananisha na Simba – kwao wanaipokea tofauti kwa sababu hao ni wapinzani wao wakubwa, kila mtu anajua hizo timu mbili za Kariakoo hazipikiki katika chungu kimoja.
Ni kweli, Kamwe alizungumza juu ya viongozi wa Serikali kuelekea mchezo wa jana, lakini chanzo kilikuwa kauli ya RC Chacha kuihusisha mechi hiyo na Simba, wapinzani wao.
“Cha kwanza, sisi kama klabu ya Yanga na sisi kama viongozi wenu na wanachama wote hapa, sisi tunamuheshimu sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Suluhu Samia Hassan. Naomba mummpigie makofi Dakatri Samia Suluhu Hassan. Tunamuheshimu kwa sababu, mtu wake aliyemtuma huku, anatuchukonoa. Huyu mtu wake ambaye Mheshimiwa Rais kamtuma huku, anatuchokonoa. Anatutafuta la rohoni sisi Yanga. Sasa kiheshima tunaanza kwanza kuomba radhi kwa aliyemtuma huku.
Baada ya radhi, tunashughulika naye, tumuambie Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, anaitwa nani? Anaitwa Paul Chacha. Jumatano atachacha kweli, yeye na hao wanaomdanganya,” alisema Kamwe akijibu matamshi ya Mheshimiwa Chacha awali.
Kama RC Chacha angetoa ahadi tu kwa wachezaji wa Tabora United bila kuhusisha ubora wa Yanga na Simba – hapana shaka Kamwe asingemtaja – kwa sababu ingekuwa sawa na Wakuu wengine wote wa Mikoa ambao hutekeleza majukumu yao ya kimkoa katika michezo ikiwemo kuhamasisha timu zao zishinde.
Kwa wapembuzi wa mambo, pamoja na kumtaja Mheshimiwa Rais Dk. Samia – bado maneno ya Kamwe hayana ukakasi kwa RC Chacha wala yeyote miongoni mwa viongozi wa Serikali anaotuhumiwa kuwatolea maneno machafu.
Kidogo labda pale aliposema; “. Jumatano (Paul Chacha) atachacha kweli, yeye na hao wanaomdanganya,”.
Neno wanaomdanganya linaweza kuleta mjadala kidogo. Akina nani? Majibu hayawezi kutosha, labda kwa maswali pia. RC Chacha kajuaje Simba ni bora kuliko Yanga?
Kwa sababu Simba imeifunga Tabora nje, ndani.
Kwani Tabora United ndio kipimo cha ubora wa Simba na Yanga?
Mbona Yanga ndio mabingwa mtetezi?
Na wanaongoza Ligi.
Na wameifunga Simba mfululizo msimu wa tatu sasa.
Yote yaliyotokea ilikuwa kuelekea mchezo wa jan. Yalikuwa mambo ya kiuanamichezo tu, ambayo yangemalizwa kimichezo na si kwa mtu kuswekwa rumande.
Kuna wakati viongozi wetu wanaacha maswali mengi kwa wanaanchi juu ya utendaji wao, hususan katika matumizi ya madaraka yao.
Kama hivi yaani, utani utani tu wa mpira, mtu kalala rumande. Na hatujui hili litamlizwaje.

0 comments:
Post a Comment