Monday, April 14, 2025

    TANZANIA YAPANGWA KUNDI A NA MISRI, ZAMBIA NA AFRIKA KUSINI AFCON U20


    TANZANIA imepangwa Kundi A katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka (AFCON U20) zinazotarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 27 hadi Mei 18, mwaka huu pamoja na wenyeji, Misri, Zambia, Sierra Leone na Afrika Kusini.
    Katika droo iliyofanyika jana makao makuu ya Chama cha Soka Misri (EFA) Jijini Cairo, mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Nigeria waliotwaa mara saba taji hilo wameangukia Kundi B pamoja na Tunisia, Kenya na Morocco.
    Nao mabingwa watetezi, Senegal wameangukia Kundi C wakiwa pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Ghana.
    Washindi wawili wa makundi yote wataungana na washindi wa tatu bora wawili wa makundi yote kwenda Hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo itakayofikia tamati Mei 18.
    Ikumbukwe timu nne zitakazofanikiwa kufika hatua ya Nusu Fainali moja kwa moja zitakuwa zimejikatia tiketi ya kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia za FIFA U-20 zitakazofanyika nchini Chile baadaye mwaka huu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YAPANGWA KUNDI A NA MISRI, ZAMBIA NA AFRIKA KUSINI AFCON U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry