
TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kengold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Lambert Sabiyanka dakika ya 11, Beno Ngasa dakika ya 39 na Adam Adam dakika ya 59, wakati bao pekee la Kengold limefungwa na Hubert Lukindo dakika ya 65.
Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya 14, wakati Kengold inabaki na pointi zake 16 nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi ya timu 16 baada ya timu hizo zote za Mbeya kucheza mechi 26.
Ligi Kuu inashirikisha timu 16 na mwisho wa msimu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment