Sunday, April 06, 2025

    TANZANIA PRISONS YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 SOKOINE


    WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Bao pekee la Tanzania Prisons leo limefungwa na winga Haroun Othman Chanongo dakika ya 61 ya mchezo huo.
    Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons wanafikisha pointi 21, ingawa wanabaki nafasi ya 15 wakizidiwa pointi moja na Kagera Sugar baada ya wote kucheza mechi 25.
    Ligi Kuu inashirikisha timu 16 na mwisho wa msimu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry