Sunday, April 06, 2025

    SINGIDA BLACK STARS YAIKANDA AZAM FC 1-0 UWANJA WA LITI


    WENYEJI, Singida Black Stars wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao pekee la Singida Black Stars leo mshambuliaji Mkenya, Elvis Baranga Rupia dakika ya 75.
    Kwa ushindi huo, Singida Black Stars wanafikisha pointi 50, ingawa wanabaki nafasi ya tatu wakizidiwa pointi moja na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 25.
    Wote wapo nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 61 baada ya kucheza mechi 23 na Simba SC yenye pointi 57 za mechi 22.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAIKANDA AZAM FC 1-0 UWANJA WA LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry