TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na nyota kutoka Ghana, mshambuliaji Jonathan Sowah dakika ya 30, beki Kwabena Frank Assinki dakika ya 56 na kiungo, Emmanuel Kwame Keyekeh dakika ya 71.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 47 katika mchezo wa 24 ingawa inabaki nafasi ya nne nyuma ya Azam FC yenye pointi 48 baada ya kucheza mechi 23, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 28 za mechi 24 sasa nafasi ya saba.
0 comments:
Post a Comment