TIMU ya Simba SC imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Al Masry katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa New Suez mjini Ismailia.
Mabao ya Al Masry leo yamefungwa na washambuliaji Mualgeria, Abderrahim Deghmoum dakika ya 16 na Mnigeria, John Okoye Ebuka dakika ya 89.
Timu hizo zitarudiana Jumatano ijayo, Aprili 9 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla kati ya Stellenbosch ya Afrika Kusini na Zamalek ya Misri katika Nusu Fainali.
0 comments:
Post a Comment