// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PAMBA JIJI YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 KIRUMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PAMBA JIJI YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 KIRUMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Saturday, April 05, 2025

    PAMBA JIJI YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 KIRUMBA


    WENYEJI, Pamba Jiji wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Bao pekee la Pamba ‘TP Lindanda’ limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Namungo FC, James Mwashinga dakika ya 21.
    Kwa ushindi huo, Pamba Jiji inafikisha pointi 26 na kusogea nafasi ya 10, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 37 nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 25.
    Ligi Kuu inashirikisha timu 16 na mwisho wa msimu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBA JIJI YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry